Prince Harry na William wakanusha taarifa za kuvutana kwao - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!

KABATA2

Monday, 13 January 2020

Prince Harry na William wakanusha taarifa za kuvutana kwao



20170823-diana-postWajukuu wa Malkia nchini Uingereza William na Harry wameipuuza ripoti ya gazeti moja hii leo inayozungumzia kuwepo mvutano mkubwa katika uhusiano wao, wakisema taarifa hiyo ni ya kukera na ya uharibifu mkubwa wakati wakirejea kwenye mazungumzo kuhusiana na mustakabali wa ufalme huo wa Uingereza.
Ndugu hao wawili walitowa taarifa isiyokuwa ya kawaida hata wakati Malkia Elizabeth wa Pili anapojiandaa kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na mwanamfalme Harry kwa mara ya kwanza tangu alipotangaza pamoja na mkewe Meghan mpango wao wenye utata wa kutaka kuyaachia majukumu ya taasisi hiyo ya kifalme.
Mkutano huo wa aina yake wa kifamilia unalenga kuweka mwelekeo wa mustakabali wa wanandoa hao.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad