Maelezo yanaibuka ya video inayosambaa ya mwanaume akichomwa moto na vikosi vya usalama akiwa hai katika eneo la Benishangul-Gumuz magharibi mwa Ethiopia, eneo la bwawa kubwa la Blue Nile ambalo lilianza kuzalisha umeme mwezi uliopita.
Katika taarifa yake siku ya Jumapili, serikali imeteua Tume ya Haki za Kibinadamu ya Ethiopia ilisema tukio hilo lilifuatia shambulio la washambuliaji wenye silaha na kusababisha vifo vya raia watatu waliokuwa wakisafiri kwenda kwenye bwawa hilo na takriban maafisa 20 wa salama walikuwa wakiwasindikiza.
Baadhi ya watu waliokuwa na silaha pia waliuawa katika mapigano yaliyofuata, tume hiyo ilisema. Waliwatuhumu raia 8 wa kabila la Tigray wanaoishi katika eneo hilo kuunga mkono mashambulizi ya kuvizia, vikosi vya usalama viliwapiga risasi na kuwaua huku raia wengine wawili waliopinga hatua hiyo pia wakiuawa, tume hiyo iliongeza.
Miili ya waliofariki ilipelekwa katika msitu wa karibu na kuchomwa moto sambamba na mtu mwingine wa kabila la Tigray ambaye alipatikana amejificha akiwa amechomwa moto akiwa hai, kwa mujibu wa tume hiyo.
Wanajeshi wa jeshi la kitaifa, vikosi vya kikanda kutoka Amhara na Southern Ethiopian Nations, Nationalities and Peoples (SNNP) wanafanya kazi katika eneo hilo, ilisema taarifa hiyo.
Ofisi ya mawasiliano ya serikali ilitoa taarifa siku ya Jumamosi kulaani mashambulizi hayo na kuapa kuwawajibisha wahusika. Lakini kutokana na mauaji mengi ya kiholela - yaliyonaswa na kamera - katika miaka michache iliyopita bila kuadhibiwa, wengi kwenye mitandao ya kijamii walionyesha mashaka.
Haijabainika iwapo kisa hicho kinahusiana na vita vya kaskazini mwa Ethiopia vilivyoanza miezi 16 iliyopita.
No comments:
Post a Comment