Takriban watu 35 wameuawa na 134 kujeruhiwa katika shambulio la kombora la Urusi kwenye kituo cha mafunzo ya kijeshi magharibi mwa Ukraine, Gavana wa mkoa wa Lviv amesema.
Kiongozi wa Kanisa Katoliki ulimwenguni, Papa Francis amelaani vikali shambulio la Urusi dhidi ya Ukraine.
"Kwa jina la Mungu, acha kilio cha watu wanaoteseka kisikike, na milipuko ya mabomu na mashambulio yakome," alisema wakati wa sala yake ya kila Jumapili kwenye uwanja wa St Peter's Square huko Vatican.
Katika mji uliozingirwa wa kusini-mashariki wa Mariupol - ambao umekuwa ukishambuliwa bila huduma muhimu na vifaa kwa karibu wiki mbili, baraza la jiji linasema wakazi 2,187 sasa wameuawa.
Maafisa wa eneo hilo walisema kumekuwa na takribani mashambulizi 22 ya Urusi kwenye jiji hilo katika siku iliyopita.
"Watu wamekuwa katika hali ngumu kwa siku 12. Hakuna umeme na maji, hakuna mawasiliano ya simu. Akiba ya mwisho ya chakula na maji inaisha," taarifa ilisema.
Vikosi vya Urusi vimeteka viunga vya mashariki mwa mji huo.
Picha za hivi majuzi za satelaiti zinaonesha uharibifu mkubwa wa miundombinu ya makazi na kiraia.
Mengi zaidi unayoweza kusoma
TANGAZAO LA KUIUZA CHELSEA:Chelsea: Roman Abramovich anasema ana mpango wa kuiuza klabu hiyo
MATAJIRI WENGINE URUSI:Urusi na Ukraine: Wafahamu wanaume mabilionea wa Urusi wanaokabiliwa na vikwazo vya dunia kwa kuwa na ushirika na Putin
"Kwa jina la Mungu, nakuomba, acha mauaji haya."
Ulipuaji wa mabomu kwa hospitali za watoto na malengo ya kiraia ni "unyama" na "hakuna sababu halali ya kimkakati", Papa aliongeza.
Waandamanaji wanaopinga vita wakamatwa nchini Urusi
Maandamano ya kupinga vita kwa mara nyingine tena yanafanyika duniani kote, ikiwa ni pamoja na Urusi - ambapo mkosoaji mkubwa wa Kremlin, Alexei Navalny ametoa wito kwa watu huko kuchukua msimamo dhidi ya Rais Putin na uvamizi wa Ukraine.
Polisi waliwakusanya baadhi ya waandamanaji katikati mwa Moscow.
Msaada kwa Mariupol ni kipaumbele cha Ukraine, anasema Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kazi muhimu zaidi iliyopo ni kupeleka msaada katika mji unaozingirwa wa Mariupol.
Alisema msafara wa misaada ya kibinadamu ulikuwa kilomita 80 tu - karibu saa mbili kwa gari - kutoka mji huo, ambao umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara na vikosi vya Urusi kwa karibu wiki.
"Tunafanya kila kitu kuvunja upinzani wa wakaaji, ambao wanazuia hata makasisi wa Kanisa la Orthodox," Zelensky aliandika, katika chapisho kwenye Facebook.
No comments:
Post a Comment