Urusi yaishambulia Ukraine:Mengi zaidi

Imechukua chini ya wiki mbili kwa herufi "Z" kupata umaarufu miongoni mwa wale wanaounga mkono uvamizi wa Rais Putin.

Katika jiji la Kazan lililopo eneo la kati la Urusi, watoto wapatao 60 na wafanyikazi katika hospitali ya wagonjwa walipigwa picha kwenye theluji na kuunda jitu "Z" mbele ya jengo lao.

Children and staff at a hospice spelling out "Z" in the open air
1px transparent line

Nadharia nyingi zimetolewa kuhusu maana ya ishara ya "Z". Ilianza kuvutia kwenye mitandao ya kijamii baada ya vifaru vya Urusi vilivyokuwa na herufi "Z" pembeni kuonekana zikielekea Ukraine.

Mwanzoni, ilidhaniwa herufi "Z" ilikuwa nambari "2" - inawakilisha tarehe 22 Februari (22/02/2022). Hiyo ndiyo siku ambayo Urusi iliidhinisha makubaliano ya "urafiki, ushirikiano na usaidizi wa pande zote" na maeneo ya Donetsk na Luhansk yaliyojitangazia kujitenga mashariki mwa Ukraine - .

Lakini sasa inaaminiwa kuwa ishara hiyo inatumiwa na wanajeshi wa Urusi kutambua vikosi vyao.

Wiki iliyopita, watazamaji wa kipindi cha habari kwenye Channel One inayodhibitiwa na serikali ya Urusi waliambiwa kuwa "Z" ilikuwa alama ya kawaida kwenye zana za kijeshi za Urusi. Tovuti ya Wakristo wa Orthodox inayomuunga mkono -Putin Tsargrad iliwaambia wasomaji alama rahisi inayotumiwa "kuepuka makabiliano ya kirafiki" na haiwezi "kuchanganyika na kitu kingine chochote".

Mkongwe wa kikosi maalum cha Urusi Sergey Kuvykin aliiambia tovuti ya jarida la Urusi, Life, kwamba alama tofauti ziliashiria vitengo tofauti vya kijeshi. "Alama kama hizi hutumika - 'Z' katika mraba, 'Z' katika mduara, 'Z' yenye nyota au 'Z' peke yake." Alisema alama hizo zilisaidia kuhakikisha kwamba askari ambao huenda hawana njia ya hawawasiliani na wenzao, wako pale wanapopaswa kuwa.

Ndege za kivita za Urusi zinaruka haraka sana kuona alama nyeupe zilizopakwa, Lt Kanali wa Jeshi la Wanahewa la Marekani, Lt Kanali Tyson Wetzel - mshirika mkuu wa Jeshi la Wanahewa katika shirika la The Atlantic Council - aliiambia tovuti ya Task and Purpose. Lakini alikubali "Z" zilikuwa "hatua ya kumaliza migogoro ili kuzuia mauaji ya ndugu" -katika makabiliano ya kirafiki kutoka kwa helikopta za mashambulizi ya Kirusi au silaha.

Russian military vehicles with "Z" on them
1px transparent line

Kusambaa kwa herufi "Z" nchini Urusi hakutokanai na mitandao ya kijamii pekee - anaonya Aglaya Snetkov kutoka UCL.

"Pia imesukumwa na serikali."

Mwanasiasa mmoja wa Urusi, Maria Butina, alishiriki mtandaoni video ya jinsi ya kuandika alama ya "Z" kwenye koti la biashara - Bi Snetkov anaeleza - "ili uingie kazini na kuionyesha kwa kila mtu bila kupiga kelele juu yake."

Lakini Aglaya Snetkov anasema ishara hiyo haipaswi kuonekana kama ya siasa za kuunga mkono mrengo wa kulia. "Kuna meme nyingi zinazobadilisha 'Z' kuwa swastika, lakini hiyo inafanywa na watu ambao wanataka kurudi nyuma dhidi ya serikali."

Na alama zingine zinatokea pia.

Herufi "V" kwa mfano -ambayo pia haipo katika alfabeti ya Cyrillic - inaonekana katika machapisho kwenye akaunti rasmi ya Instagram ya idara ya ulinzi ya Urusi, pamoja na picha za "Z".

Kuna maelezo yaliyoandikwa. "Za PatsanoV" husoma kama moja, ikimaanisha "kwa vijana" - wakati nyingine inasema "Sila V pravde", ambayo hutafsiri kwa Kiingereza kama "nguvu katika ukweli.

Nadharia moja ni kwamba herufi mbili za Kilatini zinaweza kuashiria "vostok", ikimaanisha mashariki, na "zapad", ikimaanisha magharibi. Lakini kwenye mitandao ya kijamii, pia imependekezwa kuwa jeshi la Ukraine linaamini kwamba "Z" inarejelea "Vikosi vya Mashariki" vya Urusi - na "V" kwa "kikosi cha jeshi la majini".

Instagram images of "Zs" and "Vs" from the Russian defence ministry