Picha ya zamani isiyo na rangi (black and white) ambayo baadhi ya watu kwa kupotosha wanadai inamuonyesha rais wa Urusi Vladimir Putin akitoa mafunzo kwa harakati za ukombozi kusini mwa Afrika, imekuwa ikisambaa.
Imekuwa ikitumiwa na baadhi ya watu kuhalalisha dhana ya kwa nini nchi za Afrika zinapaswa kuiunga mkono Urusi katika vita nchini Ukraine.
Picha hiyo pia iliwekwa kwenye mtandao wa Twitter na mtoto wa rais wa Uganda Yoweri Museveni.
Unaweza kusoma pia:
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Lakini haionyeshi Bwana Putin akiwa barani Afrika, na wakati ambao watu wanadai ilipigwa pia si sahihi.
Haipatikani tena
Tazama zaidi katika TwitterBBC haihusiki na taarifa za kutoka mitandao ya nje.Mwisho wa Twitter ujumbe, 1
Putin hakuwepo Tanzania
Picha hiyo ilisambazaa sana mtandaoni baada ya kuchapishwa katika blogu moja ya Zimbabwe mwishoni mwa mwaka 2018.
Machapisho hayo kwenye mtandao yalidai picha hiyo inamuonyesha Putin akiwa katika kambi ya mafunzo ya kijeshi ya Tanzania katika harakati za uhuru wa kusini mwa Afrika mwaka 1973.
Pia waliokuwepo katika picha hiyo, ilidaiwa kuwa ni Rais wa Msumbiji Samora Machel na Emmerson Mnangagwa, ambaye sasa ni rais wa Zimbabwe.
"Putin alikaa Tanzania kwa miaka minne na kutoa mafunzo kwa wapigania uhuru kuanzia mwaka 1973 hadi 1977," blogu hizo pia zilidai.
Hata hivyo, hakuna ushahidi wowote kutoka kwenye kumbukumbu za Urusi au Afrika kuhusu Putin, ambaye alizaliwa mwaka 1952, kwamba aliwahi kwenda barani humo katika miaka ya 1970.
Wasifu wa Putin kwenye tovuti ya Kremlin unaonyesha kwamba alikuwa akisoma katika Chuo Kikuu cha Leningrad State wakati huo, na kuhitimu mwaka 1975.
"Madai hayo ni ya kijinga tu," anasema Paul Fauvet, mwandishi wa habari ambaye ameishi Msumbiji kwa miongo kadhaa.
Mafunzo yaliyotolewa kwa wapiganaji wa uhuru wa Msumbiji katika makambi nchini Tanzania, anasema, "yalifanywa na wakufunzi wa Kichina na sio Wasovieti".
Pia, Mnangagwa asingeweza kuwa nchini Tanzania mwaka 1973 kwa kuwa alikamatwa mwaka 1965 na kufungwa jela kwa miaka 10 na serikali ya wazungu wa Rhodesia ya Kusini.
Je ilikuwa ziara ya Urusi nchini Msumbiji katika miaka ya 1980?
Mwandishi wa Zimbabwe Renato Matusse alitumia picha hiyo katika kitabu chake cha mwaka 2018, ambapo anasema inaonyesha Bwana Machel akiwa na washauri wa kijeshi wa Urusi wakitembelea kituo cha kijeshi karibu na mji mkuu wa Msumbiji Maputo katikati ya miaka ya 1980.
Lakini anasema ni wazi kwamba Putin hausiki.
Bwana Putin alikuwa akifanya kazi kama wakala wa KGB huko Ujerumani Mashariki kati ya 1985 na 1990 mwanzoni angelikuwa ni afisa wa ngazi ya chini, ambaye isingewezekana kuongoza ujumbe mkubwa hivyo.
Pia hakuna mahali ametajwa na Ikulu ya Kremlin kwamba aliwahi kutembelea Msumbiji, au katika sehemu yoyote ya wasifu wake.
José Milhazes, mwanahistoria na mwandishi wa habari, anaeleza kwamba mtu aliyeonekana kwenye picha hiyo alikuwa afisa mwingine mwandamizi wa Soviet aliyehudumu kusini mwa Afrika.
"Kwa kufanana kwao, naweza kusema tu kwamba ni bahati mbaya," anasema.
Georgi Derluguian, ambaye alifanya kazi kama mkalimani wa Kireno na Urusi katika miaka ya 1980, na sasa ni profesa katika Chuo Kikuu cha New York, Abu Dhabi, anasema madai kwamba mtu anayeoneka katika picha hiyo ni Putin "ni utani".
Anasema buti zilizovaliwa zinaonyesha kuwa mtu huyo ni mwanajeshi, wakati Putin alikuwa afisa wa ujasusi. Picha hiyo inamuonyesha ni kama baba yake Putin (mtu mzima).
Na jambo linguine la kuongezea kwenye utata wa picha hiyo ni kwamba mtu anayeonekana katika picha hiyo amevaa saa katika mkono wake wa kushoto. Bwana Putin - angalau siku hizi - ana kawaida ya kuvaa saa kwenye mkono wake wa kulia.
No comments:
Post a Comment