Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 14.03.2022: Coutinho, Haaland, Traore, Puig, Wirtz, Di Maria - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Sunday, 13 March 2022

Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 14.03.2022: Coutinho, Haaland, Traore, Puig, Wirtz, Di Maria

 

Coutinho

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Coutinho

Aston Villa ina kipengele cha kumnunua mbrazil anayecheza kwa mkopo klabuni hapo Philippe Coutinho lakini Arsenal inamtaka nyota huyo mwenye miaka 29 kutoka Barcelona msimu huu wa majira ya joto kama hatajiunga moja kwa moja katika kikosi cha Steven Gerrard. (Sport - in Spanish)

Erling Braut Halaand

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Erling Braut Halaand

Kipaumbele cha Erling Braut Haaland katika dirisha la kiangazi ni kuelekea Hispania kujiunga na Real Madrid au Barcelona, licha ya ripoti za mwishoni mwa wiki kudai kwamba mshambuliaji huyo Mnorway wa Borussia Dortmund mwenye umri wa miaka, 21, amekubali mpango wa kujiunga na Manchester City. (Sport)

Rais wa Barcelona Joan Laporta anasema klabu hiyo hatamsajili Haaland katika dirisha la kiangazi kama uhamisho wake utawaweka vigogo hao wa Hispania kwenye hatari ya mgogoro wa kifedha. (TV3, via Goal)

Adama Traore

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Barcelona wanataka kumsajili moja kwa moja winga wà Hispania anayecheza klabuni hapo kwa mkopo Adama Traore, 26, kutoka Wolves katika dirisha la kiangazi na wanaweza kumtoa kiungo mhispania Riqui Puig, 22, kufanikisha mpango huo. (90Min)

Wasaka vipaji kutoka Manchester United, Liverpool na Newcastle wamekuwa wakimfuatilia nyota wa kimataifa wa Ujerumani anayechezea Bayer Leverkusen Florian Wirtz lakini kiungo huyo mshambuliaji, 18, amepata majeraha makubwa yatakayomuweka nje ya uwanja msimu mzima. (Express)

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Di Maria

Winga wa Argentina Angel di Maria, 33, ameamua kwamba anataka kuondoka Paris St-Germain msimu huu na anaweza kurejea Benfica. (AS - in Spanish)

Kocha Mauricio Pochettino na mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 23, ni miongoni mwa majina makubwa yatakayoondoka Paris St-Germain msimu huu. (L'Equipe, via Mirror)

Zinedine Zidane anatajwa huenda akamrithi Pochettino kama kocha wa PSG na tayari ameanza kuangalia wa kuwasajili kutoka klabu yake ya zamani ya Real Madrid, akiwemo kiungo Mbarazil Casemiro, 30. (El Nacional - in Catalan)

Arturo Vidal, 34 anajiandaa kutimka Inter Milan msimu huu, huku klabu ya Flamengo ikionyesha nia ya kumrejesha Amerika Kusini kiungo huyo wa Chile. (Calciomercato - in Italian)

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Adrien Rabbiot

Juventus iko tayari kumuuza kiungo mfaransa Adrien Rabiot, 26, msimu huu. (Calciomercato - in Italian)

Roma wanajiandaa kupeleka ofa msimu huu kwa ajili ya mlinzi wa pembeni wa Barcelona mmarekani Sergino Dest, 21. (Corriere dello Sport - in Italian)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here