Takriban watu sita wauawa katika mlipuko DRC - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Friday, 8 April 2022

Takriban watu sita wauawa katika mlipuko DRC

 

C

Takriban watu sita waliuawa na wengine 15 kujeruhiwa baada ya mlipuko katika baa katika kambi ya kijeshi ya Katindo huko Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Wizara ya mawasiliano ilituma ujumbe wa Twitter siku ya Alhamisi usiku kuwa idadi ya waathiriwa ilikuwa ya awali, huku ikirekebisha idadi kubwa ya vifo iliyotangazwa na msemaji wa serikali Patrick Muyaya.

Miongoni mwa wahasiriwa ni kanali luteni na mkewe, kapteni, mmiliki wa baa hiyo na rafiki yake, pamoja na kijana wa miaka 12.

Uchunguzi umeanzishwa kuhusu mlipuko huo .

Mwishoni mwa 2020, serikali ilitangaza kwamba kambi ya kijeshi ya Katindo itahamishwa nje ya jiji ili kupunguza ukaribu wake na wakazi wa Goma wa watu milioni mbili. Hili hata hivyo bado halijatekelezwa.

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo linapambana na makundi mengi ya waasi mashariki mwa nchi hiyo - lakini bado haijabainika kama mlipuko huo ulitokana na shambulizi.

Gavana wa kijeshi wa jimbo la Kivu Kaskazini ametoa wito kwa watu kuwa watulivu na kuepuka uvumi wakisubiri uchunguzi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here