Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 07.04.2022: Rice, Mbappe, Danjuma, Guardiola, Lampard, Nunez - KABATA

This is the special room for news where you need to settle with!


Breaking

Friday, 8 April 2022

Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 07.04.2022: Rice, Mbappe, Danjuma, Guardiola, Lampard, Nunez

 

m

CHANZO CHA PICHA,EPA

Paris St-Germain imempatia mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, kitita cha euro milioni 150 kwa misimu miwili ili abaki klabuni hapo. (Guillem Balague)

Old Trafford imewaambia wachezaji sita kuwa wanaweza kuondoka klabuni hapo kipindi hiki cha majira ya joto. (Mirror)

Manchester United inashughulikia pia kumsajili kiongo mwingine wa kati wa Uingereza na Leeds United Kalvin Phillips, 26. (Manchester Evening News)

Manchester United imetuma mawakala kumuangalia winga wa Villarreal Arnaut Danjuma akicheza dhidi ya Bayern Munich. Winga huyo pia anawindwa na Liverpool. (Mail)

P

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Brazil inajiandaa kumpatia meneja wa Manchester City Pep Guardiola donge nono ili awe kocha wa timu yao ya taifa. (Marca)

Bosi wa Everton Frank Lampard anaungwa mkono na mmiliki wa klabu Farhad Moshiri na bodi ya klabu ya Goodison Park, licha ya Toffees kukaa pointi moja tu juu ya eneo la kushushwa daraja la Ligi Kuu. (Mail)

Newcastle na West Ham wana mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Union Berlin na Nigeria striker Taiwo Awoniyi, 24, msimu huu wa majira ya joto. (Sun)

Arsenal wanamuwinda mlinzi wa Aston Villa's na Uingereza Ezri Konsa, 24. (Football Insider)

Wolves wamemuona kiongo wa kati wa Sporting Lisbon na Portugal Joao Palhinha, 26, kuwa anafaa ikiwa Ruben Neves akaondoka msimu huu wa majira ya joto. (GiveMeSport)

d

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Manchester United inajiandaa kuvunja rekodi yake katika usajili na kumsajili kiongo wa kati wa Uingereza Declan Rice, 23. (90 Min)

Arsenal, Manchester United na Tottenham wameambiwa kuwa watahitajika kulipa £67m ikiwa wanataka kumsajili mshambuliaji wa Uruguay Darwin Nunez, 22, kutoka klabu ya huko Portugal Benfica. (Express)

Leeds United na Brighton wanataka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Eddie Nketiah, 22. (Ekrem Konur - Fichajes)

Mlinzi wa RB Leipzig na Croati Josko Gvardiol, 20, anawindwa na Tottenham. (Athletic)

Aston Villa imeonesha nia ya kumpatia mkataba kiungo wa kati wa Brighton na Mali Yves Bissouma, 25. (Football Insider)

Spurs nao wamekubali kumsajili kiungo wa kati wa Brentford na Denmark Christian Eriksen, 30, kurudi klabuni hapo. (iNews)

Meneja wa Newcastle Eddie Howe anasema kuwa wing awa Ufaransa Allan Saint-Maximin (25) anaweza kusalia klabuni hapo mbali ya kuwa na tetesi za kuondoka. (90 Min)

Newcastle nao wameonesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala, 28. (Corriere dello Sport - in Italian)

Mshambuliaji wa Fulham na timu ya taifa ya Portugal chini ya miaka 21 (U21) Fabio Carvalho, 19, amekuali kuhamia Liverpool. (Fabrizio Romano)

T

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Barcelona na Wolves wanaweza wakakubali mkataba wa kubadilishana ambao utamfanya winga Adama Traore, 26, kufanya mkopo wake na klabu hiyo ya Uhispania kuwa wa kudumu, na kumruhusu winga wa Barca anayecheza kwa mkopo Francisco Trincao, 22, kufanya vivyo hivyo huko Wolves. (Birmingham Mail)

Mshambuliaji wa Atletico Madrid na Uruguay striker Luis Suarez, 35, yupo kwenye mazungumzo na klabu za Uturuki Fenerbahce na Besiktas. (AS - in Spanish)

Mshamuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski, 33, anataka mkataba wa miaka mitatu kama atajiunga na Barcelona msimu huu wa majira ya joto. (Sport - in Spanish)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here